lulu ya tanzania huko ugaibuni

Ni Mbwana Ali Samata maarufu kama sammagoli au popa, mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya tanzania ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo anaekipiga katika klabu ya Genk huku ubeligiji. ni mfano wa kuigwa sana kwa wachezaji wengi wa kitanzania ambao wamejaa jeuri na kulewa sifa. samata, nidham malengo na kujituma ndicho kilichomfikisha hapo alipo, mbali na kuchukua kiatu cha ufungaji bora wa klabu bingwa afrika, ubora wake uliwagusa wengi barani afrika mpaka kuamin kumpa tunzo ya uchezaji bora afrika kwa wachezaji wa ndani. Popa kama anavyoitwa na rafiki yake kipenzi na anayefuata nyayo zake Thomas Ulimwengu samatta alipofika tu katika klabu ya genk alianza kupata namba katika klabu hiyo kujituma kwake mpaka sasa amecheza mechi tisa na ana magoli manne. hakika penye nia pana njia viva sammata mungu akuongoze na daima amin mwamini yeye na heshimu malengo yako na doto zako. Macho ya watanzania na maombi yao yako juu yako wewe ni njia na mwanga kwa vizazi vijavyo na sio hiki cha Jerry Muro na Manara.  
Share:
Designed and Developed by Joel Elphas 0757 755 228 or 0655 755 228 © CENTER OF WISDOM BY KALIBULE | ronangelo | NewBloggerThemes.com