kila la kheri Young African
Mabingwa wa ligi kuu ya tanzania young african maruufu kama watoto wa jangwani kesho watoondoka majira ya alfajili kuelekea Mauritius kwenda kutupa karata yao ya kwanza katika kombe la klabu bingwa dhidi ya wenyeji wao. Akiongea na vyombo vya habari msemaji wa klabu hiyo mwenye bwebwe na maneno yasiyo mwisha Jeri Muro alisema kesho wataanza safari saa kumi na moja alfajiri kwa ndege ya kukodi, aliendelea kusema kuwa safari yao itakua ya moja kwa moja mpaka nchini Mauritius hawatapepesa macho popote pia aliwataka watanzania kuiombea yanga ili wakapate ushindi huko ugenini. Kama mtanzania mpenda soka nasema viva young afrikan ushindi wenu ni ushindi wa watanzania wote.